Posts

Cha Kutumaini sina.

Image
  1. Chakutumaini sina Ila damu yake Bwana, Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha;  Kwake Yesu na Simama,  Ndiye mwamba: ni salama  Ndiye mwamba: ni salama. 2. Njia yangu iwe ndefu Yeye hunipa wokovu; Mawimbi yakinipiga Nguvu zake ndiyo nanga. 3. Damu yake na sadaka Nategemea daima, Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha. 4. Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani Nikivikwa haki yake Sina hofu mbele zake.

Yesu Kwa imani

Image
1. Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo. 2. Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa wewe, Wokovu nipewe Nakupenda wewe, Bwana wangu. 3. Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata. 4. Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo name Nami nikwandame Siku zote.

Tafuta Daima Utakatifu

Image
1. Tafuta daima utakatifu; Fanya urafiki na Wakristo tu; Nena siku zotena Bwana wako, Baraka uombe kwa kila jambo. 2. Tafuta daima utakatifu; Uwe peke yako ukimwabudu; Ukimwangalia mwokozi wako, Utabadilishwa kama alivyo. 3. Tafuta daima utakatifu; Kiongozi wako aew Yesu tu; Katika furaha au huzuni Dumu kumfuata Yesu Mwokozi. 4. Tafuta daima utakatifu; Umtawaze Roho moyoni mwako; Akikuongoza katika haki, Hufanywa tayari kwa kazi yake.

Ewe Roho Wa Mungu

Image
  1. Ewe Roho wa Mbinguni Uje kwetu sasa. Ufanye makazi yako Ndani ya Kanisa. 2. Ndiwe mwanga, umulike Tupate jikana; Mengi kwetu yapunguka, Tujalize, Bwana. 3. Ndiwe Moto, teketeza Taka zetu zote: Moyo na iwe sadaka Ya Mwokozi, yote. 4. Ndiwe Umande, na kwako Tutaburudika, Nchi kavu itakuwa Ni yenye Baraka. 5. Roho wa Mbinguni uwe Nasi hapa chini, Mwili uufananishe Na kichwa Mbinguni.

Nina Haja Nawe

Image
  1. Nina haja nawe Kila saa; Hawezi mwingine Kunifaa.  Yesu, nakuhitaji  Vivyo kila saa!  Niwezeshe, Mwokozi,  Nakujia. 2. Nina haja nawe;  Kaa nami,  Na maonjo haya,  Hayaumi. 3. Nina haja nawe;  Kila hali,  Maisha ni bure,  Uli mbali. 4. Nina haja nawe,  Nifundishe  Na ahadi zako  Zifikishe. 5. Nina haja nawe,  Mweza yote,  Ni wako kabisa  Siku zote.

Usinipite Mwokozi

Image
  1. Usinipite Mwokozi, Unisikie; Unapozuru wengine, Usinipite.  Yesu,Yesu,  Unisikie;  Unapozuru wengine,  Usinipite. 2. Kiti chako cha rehema, Nakitazama; Magoti napiga pale, Nisamehewe. 3. Sina ya kutegemea, Ila Wewe tu; Uso wako uwe kwangu; Nakuabudu. 4. U Mfariji peke yako; Sina Mbinguni, Wala duniani pote, Bwana mwingine

Yesu Kwetu ni Rafiki

Image
  1. Yesu kwetu ni rafiki, Hwamiwa haja pia; Tukiomba kwa Babaye Maombi asikia; Lakini twajikosesha, Twajitweka vibaya; Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia. 2. Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia. Haifai kufa moyo, Dua atasikia Hakuna mwingine mwema Wa kutuhurumia; Atujua tu dhaifu; Maombi asikia. 3. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kuendelea, Ujapodharauliwa Ujaporushwa pia, Watu wange kudharau, Wapendao dunia, Hukwambata mikononi, Dua atasikia.