Taji Mvikeni

 1. Ni tabibu wa karibu;

Tabibu wa ajabu;
Na rehema za daima;
Ni dawa yake njema.

 Imbeni, malaika,
 Sifa za Yesu Bwana;
 Pweke limetukuka
 Jina lake Yesu.

2. Hatufai kuwa hai,
Wala hatutumai,
Ila kweli yeye ndiye
Atupumzishaye.

3. Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twendeni na amani
Hata kwake Mbinguni.

4. Huliona tamu jina
La Yesu Kristo Bwana,
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa.

5. Kila mume asimame,
Sifa zake zivume;
Wanawake na washike
Kusifu jina lake.

6. Na vijana wote tena,
Wapendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake.

Comments