Twamsifu Mungu

 

1. Twamsifu Mungu

kwa Mwana wa Pendo,
Aliyetufia na kupaa juu.

 Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin.
 Aleluya! Usifiwe, utubariki.

2. Twamsifu Mungu
kwa Roho Mtukufu,
Ametufunulia Mwokozi wetu.

3. Twamsifu Mwana,
aliyetufia,
Aliyetwaa dhambi akazifuta.

4. Twamsifu Mungu
wa neema yote,
Ametukomboa akatuongoza.

5. Tuamshe tena,
tujazena pendo,
Na moyoni uwashe moto wa Roho.

Comments

Popular posts from this blog

Tafuta Daima Utakatifu

Usinipite Mwokozi

Yesu Kwetu ni Rafiki